Suluhisho Kamili
Kwa Kampuni Yako

Karibu kwenye mfumo wa Smart Accounting, suluhisho lenye nguvu litakalobadilisha jinsi unavyosimamia shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uhasibu, katika kampuni au biashara yako. Tunaamini kuwa Smart Accounting itakusaidia kufikia viwango vya juu vya ufanisi na kuleta urahisi usio na kifani katika shughuli zako za kila siku.

SmartAccounting “Hesabu Hekima, Maamuzi Hekima”

Utangulizi

Katika ulimwengu wa biashara yenye ushindani, ni muhimu kwa kampuni au biashara kuwa na mfumo wa uhasibu na kiutendaji ulioimarishwa na unaoweza kukidhi mahitaji yako ya kifedha na kiutawala.

Kwa Nini SmartAccounting

Smart Accounting ni mfumo unaojibu changamoto Mbalimbali na kutoa suluhisho bora kwa kampuni au biashara yako.

Msaada wa Saa 24/6

Tunatoa huduma ya msaada kwa wateja wetu masaa 24 kwa siku, siku 6 kwa wiki. Timu yetu iko tayari kukusaidia wakati wowote unapohitaji msaada. Huduma yetu ya msaada inajumuisha majibu ya maswali yako, kutatua matatizo, na kutoa maelezo zaidi kuhusu bidhaa na huduma zetu. Tuko hapa kwa ajili yako, wakati wote.

KUHUSU SISI

SmartAccounting

Smart Accounting imetengenezwa na wataalamu wa Kitanzania kutoka kampuni ya Step Ahead Financial Consultants Ltd (SAFCO), wakiongozwa na dhamira yao ya kufanya uhasibu kuwa na mchakato rahisi na unaofaa kwa mazingira ya Kitanzania badala ya kutegemea mifumo ya nje ambayo huwezi kufanya maboresho ya ziada kwenye mfumo ili kuweza kufanikisha mahitaji ya wateja kutokana na aina ya biashara au kampuni.

Tunajitahidi kutoa huduma za kiwango cha juu ambazo zinaendana na mahitaji maalum ya kila mteja wetu.

about
FAIDA ZA MFUMO

Suluhisho Letu

Smart Accounting si tu mfumo wa kawaida wa uhasibu; bali ni mfumo wa kidigitali ambao unaleta urahisi, ufanisi, na udhibiti wa hali ya juu katika utendaji mzima wa biashara au kampuni yako. Zifuatazo ni baadhi ya sifa kuu ambazo Smart Accounting inakuletea:

Urahisi wa Matumizi
Ease of Use:

Smart Accounting inajulikana kwa urahisi wake wa matumizi na kueleweka haraka. Mpangilio wake umebuniwa kwa ustadi mkubwa na unaruhusu watumiaji kuanza kutumia mfumo mara moja bila kuhitaji mafunzo ya kina. Hii inawawezesha watumiaji kuelekeza nguvu zao kwenye shughuli muhimu za kibiashara badala ya kupoteza muda kushughulika na mifumo migumu ya kiuhasibu.

Usimamizi wa Matawi Mbali Mbali
Multiple Branches Management:

Mfumo unakuwezesha kusimamia na kufuatilia matawi yako kwa uwazi, bila kuchanganyikiwa na data kutoka matawi mengine. Na unaweza kupata ripoti za kila tawi lakini pia na za matawi yote kwa Pamoja (Consolidated reports).

Dashboard ya Kuvutia na yenye taarifa kabambe
Attractive and Comprehensive Dashboard:

Mfumo wetu wa Uhasibu wa Smart Accounting una dashboard ya kuvutia na inayofaa, inayoonyesha muhtasari wa mauzo ya siku, makusanyo ya siku, wateja wanaodaiwa, wateja waliolipa, n.k, pamoja na Summary ya Mahesabu ya Kiuhasibu (Income Statement na Balance Sheet).

Ushirikiano na Mifumo Mingine
Software Integration:

Smart Accounting inaweza kuunganishwa na mifumo mingine Pamoja na makampuni ya kifedha kama vile miamala ya kibenki na simu, ikiongeza ufanisi na kurahisisha shughuli zako za kifedha. Hii inawawezesha wateja wako kuweza kufanya malipo kupitia simu zao za mkononi kwa kutumia Programu ya Mkononi yaani Mobile Application kwa urahisi, usalama na haraka zaidi.

Ufanyaji wa Maamuzi Haraka
Quick Decision Making:

Mfumo unaruhusu kuidhinisha mchakato mzima wa malipo kwenye mfumo na kupunguza muda wa kuzungusha mafaili pamoja na kusubiri, hivyo unarahisisha mchakato mzima wa kiutendaji / kiuhasibu kwa kuweza kuidhinisha ukiwa mahali popote na muda wowote.

Ufuatiliaji wa Mauzo au mapato ya huduma yako
Monitoring of Sales or Revenue of Your Service:

Unaweza kufuatilia mauzo/mapato yako kwa undani, kupata taarifa kama vile mapato kwa bidhaa au huduma maalum, na kuchukua hatua za kimkakati kwa urahisi ili kuboresha biashara / utendaji wa kampuni yako.

Usimamizi wa Bidhaa na Hesabu
Items and Inventory Management:

Mfumo wa Smart Accounting unakuwezesha kusimamia bidhaa na hesabu kwa ufanisi mkubwa. Unaweza kusajili bidhaa mpya au huduma, kuweka kipimo cha vitengo (Units of Measure), na kufuatilia orodha ya bidhaa zako (Item List). Pia, mfumo unakuwezesha kufanya hesabu za bidhaa kwa urahisi, ikijumuisha taarifa kama hesabu ya thamani ya bidhaa (Inventory Value Summary), hesabu ya kiasi cha bidhaa (Inventory Quantity Summary), na hesabu ya faida ya bidhaa (Inventory Profit Margin). Hii inarahisisha kufuatilia upatikanaji wa bidhaa na kuhakikisha kuwa huna upungufu wa bidhaa au upotevu wa bidhaa zinazohitajika.

Usimamizi wa Rasilimali Watu na Mishahara
Human Resource and Payroll Management:

Mfumo unajumuisha huduma za usimamizi wa rasilimali watu na mishahara, ikirahisisha michakato ya malipo na kutoa taarifa za kina kwa wafanyakazi. Kupitia mfumo huu unaweza kusajili wafanyakazi, kufuatilia mahudhurio ya wafanyakazi, kufanya mipango ya likizo za wafanyakazi, kuomba uhamisho wa wafanyakazi, kuchambua maombi ya kazi kwa ufasaha zaidi (Recruitment portal), kufanya mahesabu yote ya mishahara (Automatic Payroll processing), ufuatiliaji wa mikopo ya wafanyakazi na mambo mengine ya muhimu kwenye eneo la rasilimali watu.

Usimamizi wa Manunuzi
Procurement Management:

Hii ni sehemu ya muhimu sana katika mfumo wetu ambayo inawezesha kampuni kusimamia mchakato mzima wa manunuzi kwa ufanisi kama vile Usajili wa Wauzaji (Supplier Management), Kufuatilia Ombi la Manunuzi (Tracking Purchase Requests), Kupata Nukuu na Kufanya Uamuzi wa Ununuzi (Obtaining Quotations and Making Purchase Decisions), Kuweka Agizo la Ununuzi (Placing Purchase Orders), Kufuatilia Utoaji wa Bidhaa (Monitoring Goods Dispatched/issued), Uthibitishaji wa Malipo (Supplier Payment Verification) na Ripoti mbalimbali za Manunuzi (Various Procurement Reports)

Taarifa za Uhasibu
Accounting Information:

Smart Accounting inatoa ripoti za kina kuhusu hali ya kifedha ya kampuni yako, ikijumuisha taarifa kama Mizania (Balance Sheet), Mapato Na Matumizi (Income Statement), Mtiririko wa Fedha (Cash Flow), Mabadiliko ya Mtaji (Changes in Equity) na Mchanganuo wa Kina wa Kiuhasibu (Detailed Accounting Notes). Pia unaweza kufanya usuluhisho wa kibenki (Bank Reconciliation) kwa urahisi na ufanisi mkubwa sana.

Usimamizi wa Mali za Kudumu
Fixed Asset Management:

Mfumo wa Smart Accounting unasaidia kampuni kufuatilia na kusimamia mali zake za kudumu kwa ufanisi kama vile Usajili wa Mali za Kudumu, Kufuatilia Mali na kujua mahali zilipo, Ufuatiliaji wa Matengenezo, Uwezo wa kukokotoa uchakavu (Automatic Depreciation Calculation Model), na uwezo wa kutoa ripoti mbalimbali za kiuhasibu juu ya Mali za kudumu.

Ripoti za Kina na Uchambuzi
Detailed Reports and Analysis:

Smart Accounting inatoa ripoti za kina na uchambuzi wa taarifa mbalimbali za kifedha na kiutendaji. Ripoti hizi zinajumuisha taarifa za miamala ya benki (Bank Transaction Report), kitabu cha fedha (Cash Book Report), miamala kwa kila mtumiaji (Transactions Per User Report), taarifa za VAT (VAT Reports), etc.

MWONEKANO WA MFUMO

Hizi ni Baadhi ya Picha za Mwonekano wa Mfuno

BEI ZA MFUMO

Chagua Mpango wa Bei Kulingana na Mahitaji Yako

Tunatoa suluhisho za bei zinazokidhi mahitaji yako maalum. Piga hatua mpya kwa kutumia zana zetu zinazokusaidia kuchunguza na kufanikisha malengo yako bila vikwazo.

Mpango wa Msingi

Tsh 1,000,000 kwa Mwaka

Usimamizi wa Hifadhi na Huduma:

1. Ripoti ya Muhtasari wa Thamani ya Hifadhi

2. Ripoti ya Muhtasari wa Kiasi cha Hifadhi

3. Ripoti ya Mipaka ya Faida ya Hifadhi

4. Ripoti ya Mwelekeo wa Hifadhi


Wateja na Mauzo:

1. Proforma ya Mauzo na Agizo la Mauzo

2. Risiti za Mauzo na Anuani za Mauzo

3. Ripoti ya Mapato ya Mauzo

4. Ripoti ya Mauzo kwa Bidhaa/Huduma

5. Jumla za Anuani za Mauzo kwa Mteja

6. Jumla za Anuani za Mauzo kwa Kitu

7. Madeni ya Mteja

8. Ripoti ya Muhtasari wa Wateja

9. Taarifa za Wateja - Anuani na Miamala Isiyolipwa


Wauzaji na Manunuzi:

1. Anuani ya Manunuzi

2. Agizo la Manunuzi

3. Risiti za Vitu Vilivyopokelewa

4. Ripoti ya Muhtasari wa Wauzaji

5. Ripoti za Manunuzi

6. Ripoti ya Madeni ya Wauzaji

7. Ripoti ya Manunuzi kwa Mwauzaji

8. Ripoti ya Uchambuzi wa Manunuzi kwa Kitu

9. Taarifa za Wauzaji - Anuani na Miamala Isiyolipwa


Uhasibu na Ripoti:

1. Ramani ya Akaunti - FSLI

2. Kuingiza Taarifa za Kawaida

3. Kikaratasi cha Malipo

4. Kikaratasi cha Risiti

5. Akaunti za Benki

6. Uhamishaji wa Benki

7. Miamala ya Benki

8. Salio la Jaribio

9. Ripoti ya Mapato

10. Taarifa ya Mwaka

11. Taarifa ya Mabadiliko ya Hisa

12. Taarifa za Akaunti

13. Ripoti ya Kitabu cha Pesa

14. Miamala ya Kitabu cha Kawaida

15. Usimamizi wa Mali za Kudumu

16. Ulinganifu wa Benki


Idadi ya Watumiaji:

1. Hamna Kikomo cha Watumiaji

Mpango wa Kati

Tsh 3,000,000 kwa Mwaka

Sifa zote za Mpango wa Msingi pamoja na:

Uwezo wa Kuunganishwa na Mabenki na Makampuni ya Simu:

1. Uunganishaji na Mabenki na Makampuni ya Simu

2. Uunganishaji na mifumo ya malipo ya fedha kama mabenki na makampuni ya simu, rahisisha miamala.


Uwepo wa App ya Simu:

1. Kuandaliwa kwa programu ya simu kwa ajili ya upatikanaji rahisi wa maelezo ya miamala.

2. Salio za anwani za mauzo na salio zingine.


Uwezo wa Kurekodi Miamala moja kwa moja kwenye Mfumo:

1. Urekodi wa moja kwa moja wa miamala ya simu/benki kwenye mfumo

2. Kupunguza makosa katika usimamizi wa fedha


Uwezo wa kuidhinisha nyaraka za malipo kwenye mfumo:

1. Mchakato wa idhini kamili kwa malipo ndani ya mfumo.

2. Kupunguza muda wa idhini na hati za karatasi.


Idadi ya Watumiaji:

1. Hamna Kikomo cha Watumiaji

Mpango wa Juu

Tsh 5,000,000 kwa Mwaka

Sifa zote za Mpango wa Kati pamoja na:

Huduma za Rasilimali Watu na Mishahara:

1. Huduma kamili za HR ikiwa ni pamoja na mahesabu ya mishahara.

2. Utoaji wa pay slips.

3. Tovuti ya ajira mtandaoni

4. Maombi ya likizo ya kidijitali

5. Usimamizi wa mikataba.


Uwezo wa kupanga manunuzi na uidhinishaji:

1. Mipango ya manunuzi na mchakato wa idhini wa kidijitali


Uwepo wa Tovuti ya Kampuni:

1. Tovuti ya kampuni tayari kuwekwa kwenye domain ya kampuni husika na kuingiza maudhui ya kampuni na kupokea admin portal ya tovuti hiyo.


Idadi ya Watumiaji:

1. Hamna Kikomo cha Watumiaji

work
WAGENI WALIOTUTEMBELEA

Mtazamo wa kina kuhusu wageni waliotutembelea hadi sasa

1

Leo

1

Jana

1

Wiki hii

1

Mwezi huu

1

Siku zote

WATEJA WETU

Wateja Wetu Wanasema nini Kuhusu Mfumo

SmartAccounting imenisaidia sana katika kusimamia biashara yangu. Mfumo huu ni rahisi kutumia na unanipa ripoti za kina ambazo ni muhimu kwa maamuzi ya kifedha.

testimonial
Najel Builders

Dodoma

Nimepata faida kubwa tangu nianze kutumia SmartAccounting. Mfumo huu umeniwezesha kufuatilia mapato na matumizi kwa urahisi na kwa haraka.

testimonial
DomStar

Dodoma

Nimefurahishwa sana na jinsi SmartAccounting inavyosimamia Manunuzi na Mauzo. Inafanya kazi yangu kuwa rahisi na inasaidia kuokoa muda.

testimonial
Lina Millers

Dar Es Salaam

Muonekano wa ripoti za SmartAccounting ni wa kuvutia na unaoeleweka kwa urahisi. Hii inaniwezesha kuchambua taarifa za kifedha kwa haraka na kufanya maamuzi bora.

testimonial

Mlimwa Hill Palace

Dodoma

WASILIANA NASI

Wasiliana na Timu Yetu

+255 747 762 244
Namba ya Simu